Zaburi 22

kwa maana ufalme ni wa Bwana naye hutawala juu ya mataifa.

Psalm 22:28 (UKJV) For the kingdom is the LORD's: and he is the governor among the nations.

26Maskini watakula na kushiba, wale wamtafutao Bwana watamsifu: mioyo yenu na iishi milele!

27Miisho yote ya dunia itakumbuka na kumgeukia Bwana, nazo jamaa zote za mataifa watasujudu mbele zake,

28kwa maana ufalme ni wa Bwana naye hutawala juu ya mataifa.

29Matajiri wote wa dunia watasherehekea na kuabudu. Wote waendao mavumbini watapiga magoti mbele yake, wote ambao hawawezi kudumisha uhai wao.

30Wazao wa baadaye watamtumikia yeye; vizazi vijavyo vitajulishwa habari za Bwana.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.