13basi auzuie ulimi wake na mabaya, na midomo yake kutokana na kusema uongo.
14Aache uovu, atende mema, aitafute amani na kuifuatilia.
15Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.
16Uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu, ili kufuta kumbukumbu lao duniani.
17Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote.