Zaburi 34

Mtukuzeni Bwana pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja.

Psalm 34:3 (UKJV) O magnify the LORD with me, and let us exalt his name together.

1Nitamtukuza Bwana nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.

2Nafsi yangu itajisifu katika Bwana, walioonewa watasikia na wafurahi.

3Mtukuzeni Bwana pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja.

4Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote.

5Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.