11Bali wanyenyekevu watairithi nchi na wafurahie amani tele.
12Waovu hula njama dhidi ya wenye haki na kuwasagia meno,
13bali Bwana huwacheka waovu, kwa sababu anajua siku yao inakuja.
14Waovu huchomoa upanga na kupinda upinde, ili wawaangushe maskini na wahitaji, kuwachinja wale ambao njia zao ni nyofu.
15Lakini panga zao zitachoma mioyo yao wenyewe, na pinde zao zitavunjwa.