8Katika Mungu wetu tunajivuna mchana kutwa, nasi tutalisifu jina lako milele.
9Lakini sasa umetukataa na kutudhili, wala huendi tena na jeshi letu.
10Umetufanya turudi nyuma mbele ya adui, nao watesi wetu wametuteka nyara.
11Umetuacha tutafunwe kama kondoo na umetutawanya katika mataifa.
12Umewauza watu wako kwa fedha kidogo, wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao.