15Fedheha yangu iko mbele yangu mchana kutwa, na uso wangu umejaa aibu tele,
16kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana, kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi.
17Hayo yote yametutokea, ingawa tulikuwa hatujakusahau wala hatujaenda kinyume na agano lako.
18Mioyo yetu ilikuwa haijarudi nyuma; nyayo zetu zilikuwa hazijaiacha njia yako.
19Lakini ulituponda na kutufanya makao ya mbweha, na ukatufunika kwa giza nene.