2Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi. Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila.
3Unapenda mabaya kuliko mema, uongo kuliko kusema kweli.
4Unapenda kila neno lenye kudhuru, ewe ulimi wenye hila!
5Hakika Mungu atakushusha chini kwa maangamizi ya milele: atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu kutoka hema yako, atakungʼoa kutoka nchi ya walio hai.
6Wenye haki wataona na kuogopa, watamcheka, wakisema,