10Ee Mungu, watu wako waliishi huko, nawe kwa wingi wa utajiri wako uliwapa maskini mahitaji yao.
11Bwana alitangaza neno, waliolitangaza neno hilo walikuwa kundi kubwa:
12“Wafalme na majeshi walikimbia upesi, watu waliobaki kambini waligawana nyara.
13Hata ulalapo katikati ya mioto ya kambini, mabawa ya njiwa wangu yamefunikwa kwa fedha, manyoya yake kwa dhahabu ingʼaayo.”
14Wakati Mwenyezi alipowatawanya wafalme katika nchi, ilikuwa kama theluji iliyoanguka juu ya Salmoni.