1Napenda kumtambulisha kwenu dada yetu Foibe, mtumishi katika kanisa la Kenkrea.
2Naomba mpokeeni katika Bwana ipasavyo watakatifu na kumpa msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, kwa maana yeye amekuwa msaada kwa watu wengi, mimi nikiwa miongoni mwao.
3Wasalimuni Prisila na Akila, watumishi wenzangu katika Kristo Yesu.