1 Nyakati 15

Kisha Daudi akawakusanya pamoja wazao wa Aroni na Walawi:

1 Chronicles 15:4 (UKJV) And David assembled the children of Aaron, and the Levites:

2Kisha Daudi akasema, “Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kulibeba Sanduku la Mungu isipokuwa Walawi peke yao, kwa sababu Bwana aliwachagua kulibeba Sanduku la Bwana na kuhudumu mbele zake milele.”

3Daudi akawakusanya Israeli wote huko Yerusalemu ili kulipandisha Sanduku la Bwana na kulileta hadi kwenye sehemu aliyokuwa ametengeneza kwa ajili yake.

4Kisha Daudi akawakusanya pamoja wazao wa Aroni na Walawi:

5Kutoka wazao wa Kohathi, Urieli kiongozi na ndugu zake 120,

6Kutoka wazao wa Merari, Asaya kiongozi na ndugu zake 220.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.