23Mwimbieni Bwana dunia yote; tangazeni wokovu wake siku baada ya siku.
24Tangazeni utukufu wake katikati ya mataifa, matendo yake ya ajabu miongoni mwa mataifa yote.
25Kwa kuwa Bwana ni mkuu, mwenye kustahili kusifiwa kuliko wote; yeye ni wa kuogopwa kuliko miungu yote.
26Kwa maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, lakini Bwana aliziumba mbingu.
27Fahari na enzi viko mbele yake; nguvu na utukufu vimo patakatifu pake.