71Wagershoni walipokea miji ifuatayo pamoja na maeneo yake ya malisho: Katika nusu ya kabila la Manase: walipewa Golani katika Bashani na pia Ashtarothi.
72Kutoka kabila la Isakari walipokea Kedeshi, Daberathi,
73Ramothi na Anemu, pamoja na maeneo yake ya malisho.
74Kutoka kabila la Asheri walipokea Mashali, Abdoni,
75Hukoki na Rehobu, pamoja na maeneo yake ya malisho.