1 Nyakati 7

Wana wa Isakari walikuwa: Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne.

1 Chronicles 7:1 (UKJV) Now the sons of Issachar were, Tola, and Puah, Jashub, and Shimrom, four.

1Wana wa Isakari walikuwa: Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne.

2Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Shemueli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu 22,600.

3Mwana wa Uzi alikuwa: Izrahia. Wana wa Izrahia walikuwa: Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.