2Basi watu wa kwanza kurudi kukaa kwenye milki zao katika miji yao walikuwa baadhi ya Waisraeli, makuhani, Walawi na watumishi wa Hekalu.
3Wale waliotoka Yuda, Benyamini, Efraimu na Manase ambao waliishi Yerusalemu walikuwa:
4Uthai mwana wa Amihudi, mwana wa Omri, mwana wa Imri, mwana wa Bani, wa wana wa Peresi, mwana wa Yuda.
5Wazao wa Washiloni waliorudi ni: Asaya mzaliwa wa kwanza na wanawe.
6Kwa wana wa Zera: Yeueli. Watu wa Yuda jumla yao walikuwa watu 690.