28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe.
29Kwa maana mtu yeyote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, hula na kunywa hukumu juu yake mwenyewe.
30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa.
31Lakini kama tungejichunguza wenyewe tusingehukumiwa.
32Tunapohukumiwa na Bwana, tunaadibishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu.