1 Wakorintho 12

Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule.

1 Corinthians 12:5 (UKJV) And there are differences of administrations, but the same Lord.

3Kwa hiyo nawaambieni ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho wa Mungu anayeweza kusema, “Yesu na alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kusema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho Mtakatifu.

4Kuna aina mbalimbali za karama, lakini Roho ni yule yule.

5Kuna huduma za aina mbalimbali, lakini Bwana ni yule yule.

6Kisha kuna tofauti za kutenda kazi, lakini ni Mungu yule yule atendaye kazi zote kwa watu wote.

7Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.