1 Wakorintho 14

Anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe, bali atoaye unabii hulijenga kanisa.

1 Corinthians 14:4 (UKJV) He that speaks in an unknown tongue edifies himself; but he that prophesies edifies the church.

2Kwa maana mtu yeyote anayesema kwa lugha, hasemi na wanadamu bali anasema na Mungu. Kwa kuwa hakuna mtu yeyote anayemwelewa, kwani anasema mambo ya siri kwa roho.

3Lakini anayetoa unabii anasema na watu akiwajenga, kuwatia moyo na kuwafariji.

4Anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe, bali atoaye unabii hulijenga kanisa.

5Ningependa kila mmoja wenu anene kwa lugha lakini ningependa zaidi nyote mtoe unabii. Kwa kuwa yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko anenaye kwa lugha, isipokuwa atafsiri, ili kanisa lipate kujengwa.

6Sasa ndugu zangu, kama nikija kwenu nikasema kwa lugha mpya nitawafaidia nini kama sikuwaletea ufunuo au neno la maarifa au unabii au mafundisho?

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.