1 Wakorintho 15

ya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama yasemavyo Maandiko,

1 Corinthians 15:4 (UKJV) And that he was buried, and that he rose again the third day according to the scriptures:

2Kwa Injili hii mnaokolewa mkishikilia kwa uthabiti neno nililowahubiria ninyi. La sivyo, mmeamini katika ubatili.

3Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: Kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemavyo Maandiko,

4ya kuwa alizikwa na alifufuliwa siku ya tatu, kama yasemavyo Maandiko,

5na kwamba alimtokea Kefa, kisha akawatokea wale kumi na wawili.

6Baadaye akawatokea wale ndugu waumini zaidi ya 500 kwa pamoja, ambao wengi wao bado wako hai, ingawa wengine wamelala.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.