1 Wafalme 1

Katika hili, wageni wote wa Adoniya wakainuka kwa mshtuko wa hofu na kutawanyika.

1 Kings 1:49 (UKJV) And all the guest that were with Adonijah were afraid, and rose up, and went every man his way.

47Pia, maafisa wa mfalme wamekuja ili kumtakia heri bwana wetu Mfalme Daudi wakisema, ‘Mungu wako na alifanye jina la Solomoni kuwa mashuhuri kuliko lako na kiti chake cha ufalme kiwe na ukuu kuliko chako!’ Naye mfalme akasujudu akiabudu kitandani mwake

48na kusema, ‘Ahimidiwe Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye ameruhusu macho yangu kuona mrithi juu ya kiti changu cha ufalme leo hii.’ ”

49Katika hili, wageni wote wa Adoniya wakainuka kwa mshtuko wa hofu na kutawanyika.

50Lakini Adoniya kwa kumwogopa Solomoni, akaenda na kushika pembe za madhabahu.

51Kisha Solomoni akaambiwa, “Adoniya anamwogopa Mfalme Solomoni na ameshikilia pembe za madhabahu. Anasema, ‘Mfalme Solomoni na aniapie leo kwamba hatamuua mtumishi wake kwa upanga.’ ”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.