1Samweli alipokuwa mzee, akaweka wanawe kuwa waamuzi wa Israeli.
2Mzaliwa wa kwanza alikuwa Yoeli, na la wa pili lilikuwa Abiya, nao wakatumika huko Beer-Sheba.
3Lakini wanawe hawakuenenda katika njia zake. Waliziacha wakageukia faida za udanganyifu nao wakapokea rushwa na kupotosha haki.
4Basi wazee wote wa Israeli wakakusanyika pamoja na kumjia Samweli huko Rama.