2 Wakorintho 11

Laiti mngenivumilia kidogo katika upumbavu wangu! Naam, nivumilieni kidogo.

2 Corinthians 11:1 (UKJV) Would to God all of you could bear with me a little in my folly: and indeed bear with me.

1Laiti mngenivumilia kidogo katika upumbavu wangu! Naam, nivumilieni kidogo.

2Ninawaonea wivu, wivu wa Kimungu, kwa kuwa mimi niliwaposea mume mmoja, ili niwalete kwa Kristo kama mabikira safi.

3Lakini nina hofu kuwa, kama vile Eva alivyodanganywa kwa ujanja wa yule nyoka, mawazo yenu yasije yakapotoshwa, mkauacha unyofu na usafi wa upendo wenu kwa Kristo.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.