2 Wakorintho 4

Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa;

2 Corinthians 4:8 (UKJV) We are troubled on every side, yet not distressed; we are perplexed, but not in despair;

6Kwa kuwa Mungu, yeye aliyesema, “Nuru na ingʼae gizani,” ameifanya nuru yake ingʼae mioyoni mwetu ili kutupatia nuru ya maarifa ya utukufu wa Mungu katika uso wa Kristo.

7Lakini tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili ijulikane wazi kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu wala si kwetu.

8Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa;

9twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi.

10Siku zote twachukua katika mwili kufa kwake Yesu ili kwamba uzima wa Yesu uweze kudhihirika katika miili yetu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.