2 Wakorintho 4

Siku zote twachukua katika mwili kufa kwake Yesu ili kwamba uzima wa Yesu uweze kudhihirika katika miili yetu.

2 Corinthians 4:10 (UKJV) Always bearing about in the body the dying of the Lord Jesus, that the life also of Jesus might be made manifest in our body.

8Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa;

9twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi.

10Siku zote twachukua katika mwili kufa kwake Yesu ili kwamba uzima wa Yesu uweze kudhihirika katika miili yetu.

11Kwa maana sisi tulio hai siku zote tumetolewa tufe kwa ajili ya Yesu, ili kwamba uzima wake upate kudhihirishwa katika mwili wetu upatikanao na mauti.

12Hivyo basi, mauti inatenda kazi ndani yetu, bali uzima unatenda kazi ndani yenu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.