11Tumesema nanyi wazi, enyi Wakorintho na kuwafungulieni mioyo yetu wazi kabisa.
12Sisi hatujizuii kuwapenda, bali ninyi mmeuzuia upendo wenu kwetu.
13Sasa nasema, kama na watoto wangu: Ninyi pia ifungueni mioyo yenu kabisa.
14Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?
15Kuna mapatano gani kati ya Kristo na Beliari? Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini?