19Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini Bwana alikuwa msaada wangu.
20Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.
21“Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.
22Kwa maana nimezishika njia za Bwana; sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.
23Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake.