2 Samweli 22

Wewe ni taa yangu, Ee Bwana. Bwana hulifanya giza langu kuwa mwanga.

2 Samuel 22:29 (UKJV) For you are my lamp, O LORD: and the LORD will lighten my darkness.

27kwa aliye mtakatifu unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi.

28Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini macho yako ni juu ya wenye kiburi ili uwashushe.

29Wewe ni taa yangu, Ee Bwana. Bwana hulifanya giza langu kuwa mwanga.

30Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, nikiwa pamoja na Mungu wangu nitaweza kuruka ukuta.

31“Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; neno la Bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.