29Wewe ni taa yangu, Ee Bwana. Bwana hulifanya giza langu kuwa mwanga.
30Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, nikiwa pamoja na Mungu wangu nitaweza kuruka ukuta.
31“Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; neno la Bwana halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.
32Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya Bwana? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu?
33Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.