44“Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu wangu; umenihifadhi mimi kama kiongozi wa mataifa. Watu ambao sikuwajua wananitumikia,
45nao wageni huja wakininyenyekea, mara wanisikiapo, hunitii.
46Wote wanalegea, wanatoka katika ngome zao wakitetemeka.
47“Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu! Atukuzwe Mungu, Mwamba, Mwokozi wangu!
48Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi, ayawekaye mataifa chini yangu,