2 Wathesalonike 3

Lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.

2 Thessalonians 3:15 (UKJV) Yet count him not as an enemy, but admonish him as a brother.

13Kwa upande wenu, ndugu, ninyi kamwe msichoke katika kutenda mema.

14Ikiwa mtu yeyote hayatii maagizo yetu yaliyoko katika barua hii, mwangalieni sana mtu huyo. Msishirikiane naye, ili apate kuona aibu.

15Lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.

16Basi, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa kila njia. Bwana awe nanyi nyote.

17Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Hivi ndivyo niandikavyo.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.