2 Timotheo 1

Unajua ya kuwa watu wote katika Asia wameniacha, miongoni mwao wamo Filego na Hermogene.

2 Timothy 1:15 (UKJV) This you know, that all they which are in Asia be turned away from me; of whom are Phygellus and Hermogenes.

13Shika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima yale uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Kristo Yesu.

14Ilinde ile amana uliyokabidhiwa kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.

15Unajua ya kuwa watu wote katika Asia wameniacha, miongoni mwao wamo Filego na Hermogene.

16Bwana akawahurumie watu wa nyumbani mwa Onesiforo, kwa sababu aliniburudisha mara kwa mara wala hakuionea aibu minyororo yangu.

17Badala yake, alipokuwa Rumi, alinitafuta kwa bidii mpaka akanipata.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.