1Siku ya Pentekoste ilipowadia, waamini wote walikuwa mahali pamoja.
2Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali uliotoka mbinguni ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi.
3Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao.
4Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.
5Basi walikuwepo Yerusalemu Wayahudi wanaomcha Mungu kutoka kila taifa chini ya mbingu.