Kumbukumbu 10

Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena.

Deuteronomy 10:16 (UKJV) Circumcise therefore the foreskin of your heart, and be no more stubborn.

14Mbingu, hata mbingu za juu sana, dunia na kila kitu kilichomo ndani yake, ni mali ya Bwana Mungu wako.

15Hata hivyo Bwana alikuwa na shauku na baba zako, akawapenda na akawachagua ninyi, wazao wao, kuliko mataifa yote, kama ilivyo leo.

16Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena.

17Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana, Mungu mkuu, mwenye uweza na wa kutisha, ambaye hana upendeleo na hapokei rushwa.

18Huwapigania yatima na wajane, humpenda mgeni, akimpa chakula na mavazi.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.