Kumbukumbu 20

Wakati mtakapokaribia kwenda vitani, kuhani atakuja mbele na kuhutubia jeshi.

Deuteronomy 20:2 (UKJV) And it shall be, when all of you are come nigh unto the battle, that the priest shall approach and speak unto the people,

1Mtakapokwenda vitani kupigana na adui zenu na mkaona farasi na magari ya vita na jeshi kubwa kuliko lenu, msiwaogope, kwa sababu Bwana Mungu wenu aliyewatoa kutoka Misri, atakuwa pamoja nanyi.

2Wakati mtakapokaribia kwenda vitani, kuhani atakuja mbele na kuhutubia jeshi.

3Atasema: “Sikia, ee Israeli, leo unakwenda vitani kupigana na adui zako. Usife moyo wala usiogope, usitishwe wala usitiwe hofu mbele yao.

4Kwa kuwa Bwana Mungu wenu ndiye huenda pamoja nanyi kuwapigania dhidi ya adui zenu na kuwapatia ushindi.”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.