9Unapokuwa umepiga kambi dhidi ya adui zako, jitenge na kitu chochote kisicho safi.
10Ikiwa mtu amechafuka kwa sababu ya kutokwa na shahawa usiku, inampasa atoke nje ya kambi na kukaa huko.
11Lakini jioni ikikaribia ataoga, na baada ya jua kuzama ataingia tena kambini.
12Tengeni mahali nje ya kambi ambapo mnaweza kwenda kujisaidia.
13Kama sehemu ya vifaa vyenu kuweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho.