Kumbukumbu 3

Msiwaogope, Bwana Mungu wenu atapigana kwa ajili yenu.”

Deuteronomy 3:22 (UKJV) All of you shall not fear them: for the LORD your God he shall fight for you.

20mpaka hapo Bwana atakapowapa ndugu zenu kupumzika kama alivyowapa ninyi, wao pia wamiliki ile nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, ngʼambo ya Yordani. Baada ya hapo, kila mmoja wenu anaweza kurudi kwenye milki niliyowapa.”

21Wakati huo nilimwamuru Yoshua, “Umejionea kwa macho yako mwenyewe yale yote ambayo Bwana Mungu wenu amewafanyia wafalme hawa wawili. Bwana atazifanyia falme zote huko mnakokwenda vivyo hivyo.

22Msiwaogope, Bwana Mungu wenu atapigana kwa ajili yenu.”

23Wakati huo nilimsihi Bwana:

24“Ee Bwana Mwenyezi, umemwonyesha mtumishi wako ukuu wako na mkono wako wenye uweza. Kwa kuwa ni mungu yupi aliye mbinguni au duniani anayeweza kufanya kazi na matendo makuu kama ufanyayo wewe?

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.