Waefeso 6

“upate baraka na uishi siku nyingi duniani.”

Ephesians 6:3 (UKJV) That it may be well with you, and you may live long on the earth.

1Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa kuwa hili ni jema.

2“Waheshimu baba yako na mama yako,” hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi,

3“upate baraka na uishi siku nyingi duniani.”

4Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana.

5Ninyi watumwa, watiini hao walio mabwana zenu hapa duniani kwa heshima na kwa kutetemeka na kwa moyo mmoja, kama vile mnavyomtii Kristo.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.