Kutoka 15

Maji yenye kina yamewafunika, wamezama mpaka vilindini kama jiwe.

Exodus 15:5 (UKJV) The depths have covered them: they sank into the bottom as a stone.

3Bwana ni shujaa wa vita; Bwana ndilo jina lake.

4Magari ya vita ya Farao na jeshi lake amewatosa baharini. Maafisa wa Farao walio bora sana wamezamishwa katika Bahari ya Shamu.

5Maji yenye kina yamewafunika, wamezama mpaka vilindini kama jiwe.

6“Mkono wako wa kuume, Ee Bwana ulitukuka kwa uweza. Mkono wako wa kuume, Ee Bwana, ukamponda adui.

7Katika ukuu wa utukufu wako, ukawaangusha chini wale waliokupinga. Uliachia hasira yako kali, ikawateketeza kama kapi.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.