3nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake.
4“Kama ukikutana na maksai au punda wa adui yako anapotea, hakikisha umemrudisha kwake.
5Ukiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia.
6“Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao.
7Ujiepushe na mashtaka ya uongo, wala usimuue mtu asiye na hatia au mtu mwaminifu, kwa maana sitamhesabia hana hatia yeye aliye na hatia.