2“Usifuate umati wa watu katika kutenda mabaya. Unapotoa ushahidi kwenye mashtaka, usipotoshe haki ukijumuika na umati wa watu,
3nawe usimpendelee mtu maskini katika mashtaka yake.
4“Kama ukikutana na maksai au punda wa adui yako anapotea, hakikisha umemrudisha kwake.
5Ukiona punda wa mtu anayekuchukia ameanguka na mzigo wake, usimwache hapo alipoangukia; hakikisha kuwa umemsaidia.
6“Usiwanyime haki watu wako walio maskini katika mashtaka yao.