19Kisha wakatengeneza kifuniko cha hema kwa ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.
20Wakatengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani.
21Kila mhimili ulikuwa na urefu wa dhiraa kumi, na upana wa dhiraa moja na nusu,
22zikiwa na ndimi mbili zilizokuwa sambamba kila mmoja na mwingine. Wakatengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii.
23Wakatengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani,