1Bezaleli akatengeneza Sanduku la mbao za mshita: urefu wake ulikuwa dhiraa mbili na nusu, upana wake dhiraa moja na nusu, na kimo chake dhiraa moja na nusu.
2Akalifunika kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulizungushia ukingo wa dhahabu.
3Akasubu pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine.
4Kisha akatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu.