1Kisha Bwana akamwambia Mose:
2“Simika Maskani ya Mungu, yaani Hema la Kukutania, katika siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza.
3Weka Sanduku la Ushuhuda ndani yake na ulifunike kwa pazia. Ingiza meza na kupanga vitu vyake juu yake.
4Kisha ingiza kinara cha taa na uweke taa zake juu yake.