Ezekieli 11

Mmewaua watu wengi katika mji huu na kujaza barabara zake maiti.

Ezekiel 11:6 (UKJV) All of you have multiplied your slain in this city, and all of you have filled the streets thereof with the slain.

4Kwa hiyo toa unabii dhidi yao, tabiri, Ewe mwanadamu.”

5Kisha Roho wa Bwana akaja juu yangu, naye akaniambia niseme: “Hili ndilo Bwana asemalo: Hili ndilo ninyi mnalosema, ee nyumba ya Israeli, lakini ninajua mnalowaza mioyoni mwenu.

6Mmewaua watu wengi katika mji huu na kujaza barabara zake maiti.

7“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: maiti ulizozitupa huko ni nyama na mji huu ni chungu, lakini nitawaondoa mtoke huko.

8Mnaogopa upanga, nao upanga huo ndio nitakaouleta juu yenu, asema Bwana Mwenyezi.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.