Ezekieli 23

umekuletea haya yote, kwa sababu ulitamani mataifa na kujinajisi kwa sanamu zao.

Ezekiel 23:30 (UKJV) I will do these things unto you, because you have gone a whoring after the heathen, and because you are polluted with their idols.

28“Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ninakaribia kukutia mikononi mwa wale unaowachukia, kwa wale uliojitenga nao kwa kuwachukia.

29Watakushughulikia kwa chuki na kukunyangʼanya kila kitu ulichokifanyia kazi. Watakuacha uchi na mtupu na aibu ya ukahaba wako itafunuliwa. Uasherati wako na uzinzi wako

30umekuletea haya yote, kwa sababu ulitamani mataifa na kujinajisi kwa sanamu zao.

31Umeiendea njia ya dada yako, hivyo nitakitia kikombe chake mkononi mwako.

32“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “Utakinywea kikombe cha dada yako, kikombe kikubwa na chenye kina kirefu; nitaletea juu yako dharau na dhihaka, kwa kuwa kimejaa sana.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.