Ezekieli 23

Umeiendea njia ya dada yako, hivyo nitakitia kikombe chake mkononi mwako.

Ezekiel 23:31 (UKJV) You have walked in the way of your sister; therefore will I give her cup into yours hand.

29Watakushughulikia kwa chuki na kukunyangʼanya kila kitu ulichokifanyia kazi. Watakuacha uchi na mtupu na aibu ya ukahaba wako itafunuliwa. Uasherati wako na uzinzi wako

30umekuletea haya yote, kwa sababu ulitamani mataifa na kujinajisi kwa sanamu zao.

31Umeiendea njia ya dada yako, hivyo nitakitia kikombe chake mkononi mwako.

32“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “Utakinywea kikombe cha dada yako, kikombe kikubwa na chenye kina kirefu; nitaletea juu yako dharau na dhihaka, kwa kuwa kimejaa sana.

33Utalewa ulevi na kujawa huzuni, kikombe cha maangamizo na ukiwa, kikombe cha dada yako Samaria.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.