Ezekieli 35

“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya mlima Seiri, utabiri dhidi yake

Ezekiel 35:2 (UKJV) Son of man, set your face against mount Seir, and prophesy against it,

1Neno la Bwana likanijia kusema:

2“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya mlima Seiri, utabiri dhidi yake

3na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume nawe, ee mlima Seiri, nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yako na kukufanya ukiwa na usiyekaliwa na watu wala kulimika.

4Nitaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa ukiwa. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.