17wala sikupanda kwenda Yerusalemu kuwaona hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda mara moja Arabuni na kisha nikarudi Dameski.
18Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kuonana na Kefa na nilikaa naye siku kumi na tano.
19Lakini sikumwona mtume mwingine yeyote isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana.
20Nawahakikishia mbele za Mungu kuwa ninayowaandikia si uongo.
21Baadaye nilikwenda sehemu za Syria na Kilikia.