18Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kuonana na Kefa na nilikaa naye siku kumi na tano.
19Lakini sikumwona mtume mwingine yeyote isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana.
20Nawahakikishia mbele za Mungu kuwa ninayowaandikia si uongo.
21Baadaye nilikwenda sehemu za Syria na Kilikia.
22Lakini mimi binafsi sikujulikana kwa makanisa ya huko Uyahudi yaliyo katika Kristo.