Wagalatia 5

Kwa maana ndani ya Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.

Galatians 5:6 (UKJV) For in Jesus Christ neither circumcision avails any thing, nor uncircumcision; but faith which works by love.

4Ninyi mnaotafuta kuhesabiwa haki kwa njia ya sheria mmetengwa na Kristo, mko mbali na neema ya Mungu.

5Kwa maana, kwa njia ya Roho kwa imani, tunangojea kwa shauku tumaini la haki.

6Kwa maana ndani ya Kristo Yesu, kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuleti tofauti, bali lililo muhimu ni imani itendayo kazi kwa njia ya upendo.

7Mlikuwa mkipiga mbio vizuri. Ni nani aliyewazuia msiitii kweli?

8Ushawishi wa namna hiyo haukutokana na yule anayewaita.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™ Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 Biblica, Inc. Licensed CC BY-SA 4.0. “Biblica” is a trademark registered in the United States Patent and Trademark Office by Biblica, Inc.