4Mungu akaona ya kuwa nuru ni njema, ndipo Mungu akatenganisha nuru na giza.
5Mungu akaiita nuru “mchana,” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya kwanza.
6Mungu akasema, “Iwepo nafasi kati ya maji igawe maji na maji.”
7Kwa hiyo Mungu akafanya nafasi, akatenganisha maji yaliyo chini ya hiyo nafasi na maji yaliyo juu yake. Ikawa hivyo.
8Mungu akaiita hiyo nafasi “anga.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya pili.